Mtandao wa Kijamii wa Instagram umeondoa rasmi sehemu ya “Following Activity Tab” kwa lengo la kuboresha mahusiano na usalama wa watumiaji  wake.



Sehemu hiyo ambayo ilikuwa inampa uwezo rafiki yako aliyekufuata (Follow) kwenye mtandao huo, Kujua shughuli ulizozifanya kwenye mtandao huo ikiwemo Likes, Comments na watu uliowa-follow kwenye mtandao huo.

Akitoa tangazo hilo jana Oktoba 8, 2019, Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji Instagram, Vishal Shah, Amesema sehemu hiyo imekuwa ikipokea malalamiko mengi kutoka kwa wanandoa na viongozi wa dini.

Amesema kuna kisa kimoja kilitokea, Ambapo Mama mmoja alipewa taarifa na mdogo wake wa kike ambaye alim-follow shemeji yake na kudai kuwa Mumewe (Yaani shemeji yake) analike picha za mashoga na wacheza filamu za giza.

Vishal Shah amesema mama huyo ambaye alikuwa hatumii Instagram, Alienda hadi makao makuu ya Instagram kutaka akaunti ya mumewe ifutwe.

Kisa kingine ni cha kiongozi wa Kanisa Katoliki kutoka Canada. Ambaye alikuwa anatabia ya ku-like picha zisizo za maadili pasipokujua kama followers wake wanajua.

Tayari mtandao huo kwenye baadhi ya nchi umeanza kufuta pia sehemu ya Likes, Ili kuboresha mahusiano ya watumiaji.

Feature ya “Following Tab” iliwekwa mwaka 2011 kwa lengo la kusaidia watumiaji wake kujua marafiki zao au watu maarufu waliowa-follow wamefanya nini kwa siku husika.