Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akizungumza na wananchi wenye kero mbalimbali dhidi ya serikali mjini hapa jana, ambao walimuonesha mabango ya kero hizo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani hapa mapema mwezi huu.
 Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (hayupo pichani)
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (hayupo pichani)
 Mkutano ukiendelea
 Mama akitoa kero yake kwa maofisa wa idara za serikali mkoani Singida katika mkutano huo.
Maofisa wa idara za serikali mkoani Singida, wakipokea kero za wananchi hao (hawa pichani

Na Dotto Mwaibale, Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amekutana na wananchi wenye kero mbalimbali dhidi ya serikali ambao walimuonesha mabango ya kero hizo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani hapa mapema mwezi huu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kuyaona na kupokea mabango hayo alimuagiza mkuu wa mkoa kutatua changamoto za wananchi hao ambapo jana alikutana nao akiwa na viongozi wa idara za serikali kwa ajili ya kuwasikiliza na kutafuta njia ya kuzitatua kwa pamoja.

Hata hivyo ilitokea sintofahamu baina ya wananchi hao na mkuu wa mkoa huo pale walipotakiwa kusikilizwa na viongozi wa idara za serikali ambao walishindwa kuzitatua hapo awali na kufikia uamuzi wa kumuonesha mabango waziri mkuu.

Pamoja na sintofahamu hiyo baadae wananchi hao walikubali kusikilizwa  ambapo mkuu huyo wa mkoa aliwagiza viongozi hao hasa wa Manispaa ya Singida kupanga tarehe za kukutana na wananchi hao wengi wakiwa na malalamiko ya migogoro ya ardhi.



Baadhi ya malalamiko waliyoyatoa kwa Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa ni pamoja na madai ya fidia ya viwanja namba 23 na eneo lililoko nyuma ya moja ya kiwanja cha Ginnery, kupinga rufaa ya kesi ya ardhi iliyotoleea hukumi na baraza la ardhi la wilaya ya Singida.

Madai mengine ni kiwanda cha mafuta ya alizeti kumilikiwa na wajanja wachache, kutokamilika kwa mradi wa ujenzi wa matundu ya vyoo na mabweni shule ya msingi Mtinko tangu mwaka 2017 na mkopo wa Saccos fedha kutoka NSSF 160 milion zilizokuwa wakopeshwe wanachama wamekopeshwa vigogo kutoka Singida mjini.

Mkazi wa Kata ya Mwankoko Rochard Katyani ambaye ana malalamiko ya fidia ya ardhi aliomba serikali kumaliza malalamiko ya migogoro ya ardhi ambayoimedumu kwa mda mrefu.

Kati ya migogoro 27 iliyowasilishwa kwa waziri mkuu kwa njia ya mabango migogoro zaidi ya 20 inahusu masuala ya ardhi hasa fidia baada ya ardhi za wahusika kudaiwa kuchukuliwa na serikali kwa matumizi mengine.