Miss World aingia Tanzania kwa mara kwanza, Waziri kufikisha ujumbe kwa JPM (+video)

Miss World aingia Tanzania kwa mara kwanza, Waziri kufikisha ujumbe kwa JPM (+video)

Miss World Vanessa Ponce kwa kushirikiana na Miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian wametoa elimu ya hedhi salama pamoja na kugawa taulo za kike kwa wanafunzi wanawake zaidi ya 100 wa shule ya sekondari ya Moshono iliopo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha mkoani hapa.
Vanessa ambaye ni Raia wa Mexico kwa sasa yuko Mkoani Arusha kwa ziara ya siku nne ambapo akiwa mkoani hapa amezindua mashine ya kutengeneza Taulo za kike zinazojulikana kwa jina la Uhuru Pads na kugawa taulo za kike 1000 kwa wasichana wa Shule ya Sekondari Moshono iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.