Afisa Uandiikishaji  Catherine Alex wa Kijiji cha ilongero katika Halmashauri ya Wilaya Singida Vijijini akimuandikisha Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Aysharose Mattembe kwenye daftari la Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za  mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.
 Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe akisaini katika daftari la Serikali za Mitaa Tamisemi kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.
 Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Singida Vijiji, Naomi David (kulia) akimlaki Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe alipowasili kujiandikisha.

 Wananchi wa Kata ya Ilongero wakimlaki Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe alipowasili kujiandikisha.
 Mbunge Aysharose Mattembe akiwa katika picha ya pamoja na wananchi na viongozi wa Kata ya Ilongero.
 Mbunge Aysharose Mattembe, akisalimiana na Afisa Mtendaji wa Kata ya Ilongero.

 Wananchi waliohamasishwa na Mbunge Mattembe wakisubiri kujiandikisha.
 Mbunge Mattembe akielezea umuhimu wa kuchagua viongozi wanaofaa.
Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Singida Vijiji, Naomi David akisaini baada kujiandikisha katika daftari hilo.

Na Dotto Mwaibale, Singida

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM)  Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe amewataka wananchi wa Mkoa wa Singida na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha katika daftari la Tamisemi kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.

Mattembe ametoa wito huo leo wakati alipokuwa akiwahamasisha wananchi wa Kata ya Ilongero kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ikiwa imebaki siku moja tu ya kujiandikisha.

Alisema maendeleo  ya nchi yanaanzia ngazi ya vitongoji, vijiji, kata, wilaya hadi Taifa hivyo tiketi ya kuweza kuchagua kiongozi mwenye sifa nilazima kwenda kujiandikisha ili kumchagua kiongozi anayefaa.

" Bila ya kujiandikisha haitawezekana kumchagua kiongozi mnaye mtaka hivyo wito wangu kwenu kwa hii siku moja iliyobaki kwa ajili ya kujiandikisha jitokezeni kwa wingi  vinginevyo mtapoteza haki yenu ya kumchagua kiongozi mnaye mtaka" alisema Mattembe.

Aliwataka wananchi hao kujitokeza kujiandikisha bila kujali itikadi ya vyama vyao  kwani maendeleo hayana chama yapo kwa ajili ya watu wote.