Mtangazaji Maulid Kitenge tayari amethibitisha kuwa ameshajiunga Wasafi FM akitokea redio E FM.

Inaelezwa Kitenge na wenzake watakuwa kwenye kipindi cha michezo ambacho kitaanza rasmi Jumatatu ya wiki ijayo (Jumatatu - Ijumaa) kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 5) kikijulikana kwa jina la Sports Arena.

"Asanteni E FM  kuwa nami katika wakati mzuri na mbaya. Lakini muda mwingi ulikuwa mzuri sana. Nisingekuwa chochote bila nyie. Nitamisi udugu wetu wa wakati wote ambao tulishirikiana kwenye mapambano pamoja, mmekuwa watu wa muhimu sana na mnisamehe pale nilipowakwaza," ameeleza Kitenge kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Watangazaji wengine wanaoelezwa kuungana na wawili hao Wasafi FM ni Mwanaidd Suleiman, Edo, Ahmed Abdallah na Mchambuzi Edo Kumwembe.