Mfanyakazi wa kampuni ya ndege ya Southwest Airlines amefungua kesi mahakamani akiwashutumu marubani wawili wa ndege hiyo kwa kuficha kamera katika choo cha ndege na kuwachukua picha za moja kwa moja abiria ambao walikuwa wakienda kujisaidia.

Renee Steinaker anadai kuwa aliwapata marubani hao wakati wa safari ya ndege ya mwaka 2017 kutoka Pittsburgh hadi Phoenix na kuonywa kutosema kitu kuhusu kamera hiyo ya siri ambayo inadaiwa kuwa ya kiusalama.

Hata hivyo marubani hao wamekana mashtaka hayo na kudai kwamba kulikuwa na kamera iliyokuwa ikiwachukua abiria na wafanyakazi waliokwenda msalani lakini Kampuni hiyo imesema kwamba kisa hicho kilikuwa cha kushangaza.

Marubani hao hawakuitwa na kampuni hiyo ya ndege na wanaendelea na kazi yao kawaida kulingana na mashtaka hayo.

Hata hivyo hakuna tarehe ya kusikilizwa kwa kesi hiyo imewekwa hadi sasa na marubani hao wanaendelea na safari zao kama kawaida.