Serikali ya Ethiopia jana iliwaaga makondakta 35 wa treni ambao wanakwenda China kwenye programu ya mafunzo.

Makondakta hao tayari wameshapatiwa mafunzo ya mwaka mmoja nchini Ethiopia na wataalamu wa China na sasa wamepangiwa kupata mafunzo ya miezi sita zaidi kwenye chuo cha Ufundi wa Reli cha Zhengzhou.

Akiongea kwenye hafla ya kuwaaga makondakta hao, Naibu Waziri wa Usafiri wa Ethiopia Awol Wegres amesema serikali ya Ethiopia inapanga kuwezesha mafunzo zaidi katika sekta ya usafiri wa anga na ardhini kwa wataalamu wake kwa ajili ya kuifanya sekta yake ya ugavi kuwa ya kisasa.

China ni muungaji mkono mkubwa wa progranu ya ujenzi wa miundo mbinu ya reli nchini Ethiopia, ikiwa imetoa wataalamu na fedha kusaidia kujenga reli ya umeme yenye urefu wa kilomita 756 na thamani ya dola bilioni 4 za Kimarekani ambayo inaunganisha Ethiopia isiyo na bandari hadi bandari ya Djibout