LIVE STRAIGHT TALK: The Art Of Super Respect Kudos kwa Mkurigenzi Mkuu wa EFM @majizzo kwa Ustaarabu wa ajabu aliounyesha jana wa kuagana na Mfanyakazi wake wa Miaka 5 @kitengemaulid na muhimu sana katika Station zake ambaye ameamua kujiunga na WCB sio kawaida kwa sisi Watanzania kuachana kwa amani huwa ni lazima pangekuwepo na Figisu figisu na majungu majungu mengi sana ... lakini majuzi Kitenge alitangaza kujiunga rasmi na WCB na Jana Majizzo akaiweka wazi kwamba ana amani na the moves na kwamba anamtakia mafanikio aendako ikiwa na maana kwamba anaruhusiwa pia kurudi wakati wowote akiamua anataka kurudi ...unaitwa UUNGWANA au USTAARABU ULIOPITILIZA ....

Majizzo ni mmoja wa Binadam wachache sana hapa mjini ambaye nikiwa naye tunaongea huwa ninatuliza Akili Zangu zote chini cause ni Binadam mwenye AKILI KUBWA sana so on the other hand sikushangaa pia...kwa bahati mbaya sana Mfumo wetu wa Maisha Kibongo bongo huwa hautufundishi Wanaume kuwapenda Wanawake au Kuachana kwa Aamani katika Mahusiano hasa Mapenzi sisi ikifika mwisho wa Mahusiano huwa hatuwezi kuachana kwa amani yaani Mwanaume huwezi kumuambia mtu wako kama Wazungu kuwa ....the relationship its not working lets call it a quits ....

Ingawa pia nimejifunza kuwa Mwanaume akiwa na Pesa Mwanamke hawezi kukubali kuachana kwa amani na Mwanaume akiwa hana kitu Mwanamke ana mzigo the same Mwanaume hatakubali kuachana kwa amani so kumbe tatizo ni UMASIKINI PIA halafu Wabongo tunasumbuliwa sana na Matatizo 2 tu katika Maisha yetu nayo ni WANAWAKE na PESA hapa mjini ukisikia ugomvi baina ya marafiki ujue ni mambo 2 tu PESA au WANAWAKE ...inasikitisha sana Wabongo tunafeli sana kwa mambo yasiyokuwa na msingi kabisa ndio maana Majizzo na Kitenge wanastahili pongezi kubwa sana kwa kuweka Historia mpya ya KUACHANA KWA AMANI kwanini wameachana kwa Amani ni kwa sababu Majizzo amekubali FACT OF LIFE kwamba Mfanyakazi wake anataka kusonga mbele kutafuta Pesa zaidi na Maendeleo yake zaidi na ameamua kwa sasa kwamba anaweza kuvipata WCB sasa unamzuiaje wakati alikua na wewe Miaka 5 anakujua nje ndani kwamba Ndoto zake haziwezi kufanikiwa akiwa na wewe FULL STOP! Bravo Majizzo KWA UELEWA and THIS CASE CLOSED! - @lemutuz_super