Wakati baadhi ya watuhumiwa wa kesi za uhujumu uchumi wakiwa tayari wamekiri makosa na kulipa faini na fidia Mahakamani huku wengine wakiendelea na mchakato wa mazungumzo na DPP, taarifa mpya kwa sasa ni wizi wa kompyuta kwenye ofisi za DPP.

Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa wamethibitisha kupokea taarifa ya wizi huo wa Kompyuta katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) kanda ya DSM.

Kamanda Mambosasa amesema wamepokea taarifa hiyo Jumanne asubuhi October 15, 2019 na kwamba mpaka sasa hakuna aliyekamatwa ila wanaendelea na uchunguzi kuwabaini waliohusika.