Kila mtu dunia hii anahistoria yake
Kila mtu dunia hii anahistoria yake
Kijana wa miaka 24 alikua anaangalia ktk dirisha la treni, mara akahamaki akasema…
_"Baba angalia, miti inarudi nyuma, inarudi kwa kasi sana!!"_👨🏽🚊🌳🌴🌵🌲
Baba yake akamwangalia kwa furaha kisha akatabasamu! 😊👴🏼
Wapenzi wawili waliokaa karibu nao, wakamuangalia yule kijana wa miaka 24 and kuwaza wenyewe, ni mkubwa sana ila anatabia za kijinga, lazima atakua na matatizo ya akili, ndio maana hata baba yake ahangaiki naye.😳🤔🤔
Ghafla yule kijana akashangaa tena…
_"Baba, angalia mawingu yanakimbizana na sisi!!"_
😃👨🏽 ☁🌥☁
_"Baba, angalia mawingu yanakimbizana na sisi!!"_
😃👨🏽 ☁🌥☁
Wale wapenzi wawili wakashindwa kuvumilia na kumwambia yule Mzee.
_"Kwanini usimpeleke Mtoto wako kwa daktari mzuri, pengine wa matatizo ya akili?"_ 😤 😠😡
Yule mzee akawaangalia kisha akatabasamu na kusema..
_"Ndio nimefanya hivyo, Hapa tumetoka kwa dokta, ila sio wa akili.."_😊👴🏼
Akaendelea kueleza…
_"Mwanangu alizaliwa kipofu, Leo ni siku yake ya kwanza kabisa kuona.. Tabia zake zinaweza kuwa za kijinga na kero kwenu ila kwangu ni zaidi ya miujiza"_😊😘😀🙌🏽
Wale wapenzi wawili wakatulia tulii na kuishiwa maneno huku wakibubujikwa na machozi na aaibu machoni pao…😭😭
*Kila mtu ktk dunia hii ana historia yake, usimhukumu mtu haraka kwani hufahamu wametokea wapi na wamepitia mangapi kwani ukweli kuhusu maisha yao unaweza kukushangaza. Waheshimu na kuwachukulia wepesi wenzako hata kama wewe unamaisha mazuri…*
_*Hadithi hii imenifundisha kitu kikubwa na nimeonelea niwashirikishe…*_