BAADA ya kutoalikwa kwenye sherehe mbili za mastaa wenzake, Irene Uwoya na Aunt Ezekiel, muigizaji Kajala Masanja amesema kuwa haoni tatizo na hakuna kitu kilichopungua.  Akizungumza na Amani, Kajala amesema hawezi kujisikia vibaya au kuwa mnyonge kwa sababu hujaalikwa, kwani sherehe hizo zinaisha siku moja na kusahaulika lakini maisha yake yanaendelea.

“Yaani hata nisipopewa mualiko wa kwenda kwenye pati zao, naona sawa maana wanafurahia siku moja tu, wanakuwa kwenye hali ya kawaida kwa hiyo hali hiyo hainiumizi hata kidogo,” alisema Kajala.

Hivi karibuni, Kajala hakuonekana kwenye sherehe mbalimbali za mastaa wenzake ikiwemo bethidei ya Aunt na uzinduzi wa Reality Show ya Uwoya