Msanii mkongwe wa muziki nchini Uganda, Jose Chameleone  ameweka hadharani ujumbe wa mtu anayemtishia maisha endapo atashindwa kumtumia kiasi cha pesa alichomuomba.

Chameleone kwa sasa anajihusisha na siasa nchini humo.

Kupitia ukurasa wake wa facebook msanii huyo amesema baada ya kufuatilia usajili wa namba hiyo alikutana na jina la Jenifer Maniraduha tofauti na alivyojitambulisha awali kama Generali.

“Tahadhari, nimekuwa nikipokea vitisho kutoka kwenye namba hii (akiitaja), mtu ambaye amejitambulisha kwa jina la Generali, mara ya kwanza alinitumia ujumbe  Septemba 10 saa 12 jioni na alitaka nimtumie shilingi 5,000,000 la sivyo ataniua ila nilipuuzia, leo tena amenitumia ujumbe wa kutaka 8,000,000 kama nisipotuma ataniangamiza”, ameandika Chameleon.

Video: Sister Fay afunguka hisia zake kwa Diamond ”mume bora kwangu”
Aidha Chameleone amesema kuwa hadi sasa tayari amevitaarifu vyombo vya usalama  nchini humo na wamemuahidi kufanya uchunguzi juu ya suala hilo.