Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.8 limetokea Papua mashariki mwa Indonesia.

 Kituo cha Utafiti wa Jiolojia cha Marekani (USGS), kimetangaza kuwa tetemeko hilo limetokea kilometa 138 kusini magharibi na kufikia kina cha  kilomita 10.

 Haijulikani bado ikiwa tetemeko la ardhi limesababisha uharibifu wa maisha au mali.

 Hakuna onyo la Tsunami lililotolewa.