WEKA pembeni mapito aliyoyapitia! Hawa Mayoka ‘Hawa Nitarejea’ wa sasa amekuwa mpya! Amerudi enzi zile alizokuwa akisikika na sauti ile ya Nitarejea akiwa na Diamond Platnumz.

Vibao vyake viwili; Kucheka na Shaghala Baghala vimemrudisha kwenye chati ya muziki na kwenda sambamba na wasanii wengine wa kike wanaosumbua kwenye gemu la Bongo Fleva.

NAFASI ZA 98 AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO BONYEZA HAPA


Kwa sasa Hawa amekuwa gumzo kila kona, si kwa muziki anaoufanya bali kwa kuchora tattoo yenye sura ya Diamond katika kifua chake. Mengi yameongelewa juu ya kuchora tattoo hiyo huku wengine wakidai kuwa ni kwa sababu msanii huyo ndiye aliyemtoa kwenye gemu na alipopotea ndiye aliyemrudisha na kumuweka sawa!

Mikito Nusunusu limebambana na Hawa ambapo amefunguka mengi na katika makala haya anaanika zaidi;Mikito: Hongera bwana, tattoo imekukaa poa sana!

Hawa: Nashukuru sana!

Mikito: Hivi ina muda gani vile?Hawa: (Anacheka). Ina kama mwezi mmoja na nusu hivi.

Mikito: Sasa kwa nini uliamua kuichora? Yaani sababu hasa ni nini?

Hawa: Kiukweli niliamua kuichora hii Tattoo ili kuonyesha ni kiasi gani bado nauthamini mchango wa Diamond kwenye maisha yangu. Unajua mbali na wazazi wangu, Diamond ni kama mzazi wangu wa pili. Amenisaidia sana na nyie wenyewe mnajua.Mikito: Ahaa! Vizuri lakini mbona watu wanasema kuwa umechora hiyo tattoo kwa kuwa unahitaji kurudisha majeshi kwa Mondi na kwamba hiyo ni njama tu ya kumuingia.

Hawa: Mmmh! Hakuna. Uhusiano wangu na Chibu ulishaisha muda mrefu sana, tena sasa hivi ana uhusiano wake ambao anauheshimu mno hivyo sidhani kama hayo wanayoyasema yana ukweli wowote, mimi siwezi kufanya hivyo.Mikito: Oooh! Vipi lakini kama ikitokea Diamond akahitaji kurudiana na wewe utakuwa tayari?

Hawa: Hapana, hicho kitu hakiwezekani! Pia siwezi kujibu swali ambalo bado halijatokea. Ikitokea ndiyo nitajua cha kufanya japo najua kuwa haiwezi kutokea.

Mikito: Watu wengi hasa mashabiki zako walidhani kwamba ungechora tattoo ya mama yako lakini imekuwa ndivyo sivyo.Hawa: Unajua watu wanapenda kuongea mambo ambayo hawana uhakika nayo.Tattoo ya mama yangu ipo ila nimeichora sehemu ambayo haionekani na hata hii ya Diamond mama yangu anaijua na hajasema lolote.

Mikito: Unahisi Diamond akiiona ataichukuliaje?Hawa: Sijui atakavyo ichukulia, japo mimi sijali hata kama hatofurahia lakini mimi kwangu hiyo itakuwa haina shida kwa sababu mbali na kwamba Diamond ni mtu muhimu sana kwenye maisha yangu, lakini pia inabidi atambue kuwa yeye ni mtu maarufu, hivyo mimi ni shabiki yake pia ndiyo maana sijaona ugumu wowote kuichora.

NAFASI ZA 98 AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO BONYEZA HAPA


Mikito: Mara yako ya mwisho kuwasiliana na Diamond ilikuwa lini?

Hawa: Muda mrefu sana umepita sijawasiliana naye, nadhani ni kwa sababu ya ubize alionao.