Muda mfupi baada ya msanii,  Diamond Platnumz kuwaalika Harmonize na Ali Kiba katika tamasha la Wasafi, wawili hao wameibuka na kumjibu.


Leo Jumatano Oktoba 30, 2019 Diamond wakati akizungumzia tamasha hilo litakalofanyika Novemba 9, 2019  jijini Dar es Salaam alisema ana imani Harmonize atashiriki na kwamba amepeleka mwaliko kwa uongozi wa Ali Kiba, ili msanii huyo naye ashiriki tamasha hilo.

"Wenzetu Nigeria ndio maana wanaendelea kwenye muziki kwani kunapokuwa na matamasha kama haya wanaweka tofauti zao pembeni, kumkuta jukwaa moja Wizkid na Davido ambao walikuwa na bifu kwao ni jambo la kawaida.”

“Kwa nini tung’ang’anie bifu hata sehemu ambayo ni ya kutengeneza pesa na kutuleta Watanzania pamoja,” amesema Diamond katika mkutano wake huo na waandishi wa habari.

Harmonize kwa upande wake alipoulizwa alijibu;  “achana na hayo mambo ya Diamond, tuongee mambo mengine.”