Msanii wa muziki Bongo anayefanya vizuri na ngoma yake ya Uno, Rajab Abdul Kahali maarufu kama Harmonize au Konde Boy anaendelea na ”tuor” ya kuitambulisha ngoma yake ya Uno nchi mbalimbali za Afrika.

Harmonize na Afisa Mkuu Mtendaji wa lebo ya Konde Gang, wameonyesha nia ya kutikisa anga za muziki kwa kuandaa ‘tuor’ ya kuutambulisha wimbo huo.

Lengo ni kuhakikisha wimbo huo unawafikia mashabiki zake wote Afrika.

Kufikia sasa, Konde Gang tayari wametua katika baadhi ya mataifa barani Afrika ishara ya wazi kuwa ngoma hiyo inaendelea Ku-Trend nchini Tanzania huku kila sehemu ikisikika mawimbi ya wimbo huo.

Harmonize na kundi lake tayari wamefanya utambulisho Dar es Salaam, Nairobi na Kampala huku akitazamiwa Kigali, Rwanda.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram Harmonize amekuwa akipakia matukio mbalimbali kuhusu safari yake ya kuutambulisha wimbo ‘Uno’.

Alipokuwa anatembelea vituo mbalimbali vya habari, Jijini Dar es salaam Konde Boy alisema Uno ni wimbo maalum sana kwake kwani aliuandika akiwa katika kipindi kigumu, lakini pia Uno ni moja ya ngoma zake ambazo zinatambulisha uwezo wake wa juu kwenye utunzi lakini pia kuimba.

Wale mashabiki ambao walidhani Konde Boy bila wasafi haiwezekani nadhani ngoma ya Uno ni ngoma iliyokuja kumtambulisha vyema Harmonize na kuutambulisha uwezo wake, ni ngoma yake ya kwanza kuitoa akiwa kama jeshi la mtu mmoja ambaye anaweza kufanya mambo makubwa.

Hata katika mahojiano na vituo mbalimbali vya habari Harmonize ameonesha uwezo mkubwa kifikra na katika utendaji, zaidi tu mashabiki wanatakiwa wamwamini na kumpa nafasi ili aweze kufanya kazi na kueendelea kuachia ngoma kali kama Uno.