MREMBO ambaye kwa saa anatamba na kibao chake cha Sensema akimshirikisha Whozu, Hamisa Mobeto amesema kamwe hatarajii kuacha kufanya muziki unaomuingizia pesa nyingi kisa maneno ya watu.

Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Mobeto alisema mara nyingi watu wanaokatisha wenzao tamaa ndiyo hao ukianza kufuatilia maisha yao unakuta hata baiskeli au bajaj hawana.

NAFASI ZA 98 AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO BONYEZA HAPA

“Mimi siwezi kuacha kufanya muziki kwa sababu ya maneno ya watu f’lani waliokosa kazi za kufanya, acha waseme kuwa mimi sijui kuimba mara ooh nimevamia fani lakini hawajui nia na malengo yangu ya kuingia kwenye hii fani, wala hawajui mimi nafaidika na nini,” alisema.