Mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi Regina Chonjo akionyeswa mchoro wa ujenzi wa stendi ya daladala na mhandisi mkazi mradi wa ujenzi wa stendi hiyoMhandisi Anthonio Mkinga.
 Mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi Regina Chonjo kulia akikagua vyoo 16 vinavyo jengwa kwenye eneo la mradi wa stendi ya daladala vinavyodaiwa kutumia milioni 256.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi Regina Chonjo akiongozana na wataalamu mbali mbali akikagua eneo litakalo jengwa stendi ya daladala.

Na Agrey Evarist, Morogoro.

Mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi.  Regina Chonjo ashtukia wizi wa fedha katika mradi wa ujenzi wa stendi ya magari madogo (Daladala) katika manispaa ya Morogoro baada ya kukagua jengo moja moja.

Hayo yamebainika leo baada ya mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi. Regina Chonjo kufanya ukaguzi katika mradi huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 5 na milioni 247 utakao husisha ujenzi wa stendi ya daladala, bajaji, malori, vyoo panoja na sehemu za kupumzikia abiria ambapo mkuu huyo akabaini wizi kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo katika ujenzi wa matundu 18 ya vyoo ambayo kwa maelezo unatarajiwa kutumia milioni 256 hali iliyo mshangaza mkuu huyo wa wilaya.

Baada ya kubaini madudu hayo Bi. Chonjo akawataka Takukuru, jeshi la polisi sambamba na watu wa usalama wa taifa kufanya upembuzi na kubaini wote walio husika pamoja na kufanya uchunguzi kwa aliyeingia makubaliano hayo ambapo awali mhandisi mkazi wa eneo hilo pamoja na mratibu wa miradi ya benki ya dunia (UGSP) wa manispaa ya Morogoro wakielezea mradi huo.

Ujenzi huo unaonekana kuwa na changamoto nyingi huku fedha zilizo tolewa na benki ya dunia kama mkopo na zinazotarajiwa kumlipa mkandarasi zikitakiwa kurudishwa mwishoni wa mwezi wa 12 kama hazijatumika huku kwa makuballiano ya mkataba wa ujenzi huo ukikadiriwa kukamilika mwezi wa 5 mwakani.