Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema kuwa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize ni moja ya vijana wanaofanya kazi kubwa zaidi kuitangaza Tanzania nje ya nchi na kazi za kusaidia jamii.DC Mjema akiongea kwenye uzinduzi wa msanii huyo wa ‘KONDE BOY MGAHAWA’, Amesema kitendo cha Rais Magufuli kutamani kumuona Harmonize akigombea Ubunge jimboni kwao Tandahimba, Hakukosea kwani kijana anayejitolea kusaidia jamii yake.