Mchumba wa Davido, Chioma Rowland ameamua kuufichua hadharani uso wa wao wa kiume baada ya kuanika picha za mtoto huyo katika mitandao ya kijamii.

Chioma alizianika picha hizo katika Instagram stories yake jana Alhamisi, Oktoba 24, 2019 huku zikiwavutia mashabiki wengi na kuwapongeza wachumba hao kwa kupata mtoto.


Chioma na Davido walipata mtoto wao, siku chache zilizopita na kumpa jina la David Adedeji Adeleke Jr.

Jumapili iliyopita, Oktoba 20, 2019, kupitia mtandao wa Twitter, Davido (26) alimuita
mchumba wake ‘Chioma’ kuwa ni mwanamke jasiri.


“Omoba ti de!!! David Adedeji Adeleke Jr I!! D prince is here!!!! 20 – 10 – 2019!!! Love you my strong
wife!!! I love you!!!!! ❤️��,” Davido alitwiti.Davido alimchumbia Chioma mnamo Septemba jijini London nchini Uingereza na kumvalisha pete siku 10 baadaye nyumbani kwao na Chioma jijini huko Lagos nchini Nigeria.