Msanii wa Nigeria, Davido ameingia kwenye vichwa vya habari huko nchini kwao baada ya kumpatia zawadi ya cheni msanii mwenzake aitwae Zlatan.Imeelezwa kuwa cheni hiyo yenye nembo ya 30 Bilion Gang imenunuliwa kwa pesa za Nigeria Milioni 3 Naira ambazo ni sawa na fedha za kitanzania Milioni 19.

Davido ameacha maswali yasiyokuwa na majibu kwa mashabiki huku wengine wakisema huenda Davido ana mpango wa kumsaini msanii huyo katika lebo yake.

Davido na Zlatan hapo awali walishawahi kufanya wimbo wao wa pamoja uitwao Bum Bum