Chuo Kikuu cha Kenyatta nchi Kenya kimefungwa hapo jana kwa maelezo hadi taarifa nyingine zitakapotolewa baada ya maandamano yaliyokuwa yakifanywa na Wanafunzi kuharibu baadhi ya mali za Chuo na kuleta usumbufu

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kansela Msaidizi wa Chuo hicho, Prof. Paul K. Wainaina imeeleza kuwa Baraza la Seneti limefikia uamuzi huo na Wanafunzi wote wanatakiwa kuondoka Chuoni hapo mara moja

Hata hivyo, Kiongozi wa Umoja wa Wanafunzi katika Chuo hicho, Joshua Ayika amewashauri Wanafunzi kupuuza taarifa hiyo na badala yake wasubiri taarifa kutoka kwake

Ikumbukwe Jumatatu wiki hii, Wanafunzi wakiongozwa na Joshua Ayika waliandamana kupinga kuhusu masuala mbalimbali Chuoni hapo huku wakitaka Prof. Wainaina kujiuzulu, tukio lililoleta msongamano wa magari katika barabara Kuu ya Thika baada ya Polisi kujaribu kuwazuia

Miongoni mwa mambo wanayolalamikia Wanafunzi hao ni muda mdogo wa kulipa ada uliopo, kufukuzwa kwa wafanyakazi bila taarifa ambapo Wafanyakazi 700 wameondoshwa kazini chuoni hapo, kupanda kwa ada ya Mahafali bila taarifa kutoka Ksh. 3,500 hadi Ksh. 6,000