Wadau mbalimbali wa serikali ya China, Tanzania na mitandao wakikata utepe kuashiria  uzinduzi rasmi mahusiano ya kushirikiana kubadilishana tamaduni kupitia mtandao uliofanyika leo katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
 Mtendaji Mkuu wa Shirika la Mtandao la China  Zhao Hui akizungumza kuhusu mahusiano ya Tanzania na China katika masuala ya elimu, miundombinu na kushirikiana katika tamaduni wakati wa uzinduzi rasmi wa mahusiano ya kushirikianakatika  kubadilishana tamaduni kupitia mtandao uliofanyika leo katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa kwanza wa utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania, Zhang Bing akizungumza kuhusu namna ushirikiano wa Tanzania na China ulivyoweza kuunganisha tamaduni za nchi hizo mbili wakati wa uzinduzi rasmi mahusiano ya kushirikiana kubadilishana tamaduni kupitia mtandao uliofanyika leo katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Mchekeshaji kwenye Mitandao ya kijamii Anastazia Exavery maarufu kama Ebitoke akizugumza kuhusu namna mitandao ya kijamii ilivyoweza kuinua kipaji chake wakati wa uzinduzi rasmi mahusiano ya kushirikiana kubadilishana tamaduni kupitia mtandao uliofanyika leo katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Mchekeshaji kwenye Mitandao ya kijamii  Agness Joseph, Maye Kidoti akizungumzia mafanikio aliyoyapata kupitia mitandao ya kijamii wakati wa uzinduzi rasmi mahusiano ya kushirikiana kubadilishana tamaduni kupitia mtandao uliofanyika leo katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wa masuala ya utamaduni wa Tanzania na China wakiwa kwenye ukumbi wa mkutano wakati wa  uzinduzi rasmi mahusiano ya kushirikiana kubadilishana tamaduni kupitia mtandao uliofanyika leo katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wa serikali ya China, Tanzania na mitandao wwakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa  uzinduzi rasmi mahusiano ya kushirikiana kubadilishana tamaduni kupitia mtandao uliofanyika leo katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

KAMPUNI ya Star Media, Shirika la mtandao wa China pamoja na Wizara ya habari, utamaduni, Sanaa na michezo wamezindua rasmi mahusiano ya kushirikiana kubadilishana tamaduni kupitia mtandao na hiyo ni kwa kupitia filamu na tamthiliya mbalimbali. 

Akizungumza katika hafla hiyo Mtendaji Mkuu wa Shirika la Mtandao la China  Zhao Hui amesema kuwa mahusiano ya baina ya Tanzania na China yamekuwa yakiimarika kila siku huku wakishirikiana zaidi katika masuala ya tamaduni huku mahusiano ya China na Afrika yakiendelea kukua na kudumu kila siku.

Amesema kuwa mtandao umekuwa ukiwaweka watu karibu zaidi tofauti na ilivyokuwa awali na wanaamini  azma hiyo ya kubadilishana tamaduni baina ya nchi hizo mbili utakuza mawasiliano pamoja na mawasiliano.

 Pia katibu wa kwanza wa Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini amesema mahusiano ya China na Tanzania yamezidi  kukua zaidi na hiyo ikiwa ni matokeo bora yaliyopandwa na waasisi wa mataifa hayo  ambao walipanda mbegu bora ya ushirikino, ambayo matokeo yake yanaonekana sasa hivi.

Amesema mahusiano kupitia mtandao utaimarisha mahusiano ya nchi hizo mbili huku akipongeza idadi kubwa ya  wanafunzi  wanaojifunza lugha ya kichina katika vituo vya Chuo kikuu cha Dar es Salaam na Chuo kikuu cha Dodoma.

Amesema wanafunzi hao wanaojifunza lugha hiyo wamekuwa wakitembelea nchi hiyo ili kuweza kujifunza zaidi ili kuendelea kujifunza na kudumisha mahusiano hayo yaliyodumu kwa miaka 55 sasa.

Kwa upande wake mchekeshaji maarufu nchini Ebitoke amesema kuwa mitandao ya kijamii ina nguvu sana hivyo haina budi kuitumia vizuri ili kuwezesha zaidi masuala ya kibiashara na mahusiano bora baina ya China na Tanzania.

Amesema kuwa mtandao mahusiano bora baina ya China na Tanzania yataimarika zaidi pamoja na kuelewana miongoni mwao na hiyo ni sambamba na kuendeleza mahusiano katika masuala ya biashara, elimu na tamaduni.