Cardi B Alisogeza Siku Zake Mbele iLi Afanye Mapenzi Na Offset Kwa Mara Ya 1

Cardi B Alisogeza Siku Zake Mbele iLi Afanye Mapenzi Na Offset Kwa Mara Ya 1


Cardi B ametoboa siri ya mahusiano yake na Offset, amesema aliwahi kusogeza 'Siku zake' mbele ili tu akutane kimwili na rapper huyo kwa mara ya kwanza.

Kwenye mahojiano na kipindi kipya 'Untold Stories of Hip Hop' cha mtangazaji Angie Martinez, Cardi alisema haikuwa rahisi kumkubalia Offset kwa mara ya kwanza wanakutana kwa sababu alishaweka nadhiri kwamba hatokuja kutoka kimapenzi na wasanii wa Hip Hop.

Baada ya muda kupita, Penzi likakolea pasina hata kuwahi 'Kugusana' Cardi aliona dalili pengine penzi lingepepea na alitaka kukutana kimwili na Offset.

Changamoto ilikuja kwamba alikuwa kwenye Siku zake (Period) lakini aliamua kutumia vidonge vya kukata hali hiyo kwa muda na hatimaye alitimiza lengo lake. Alikuja kumsimulia stori hiyo Offset mwezi mmoja baadaye.