Bondia aliyepata matatizo ya ubongo katika pambano afariki

Bondia aliyepata matatizo ya ubongo katika pambano afariki

Bondia wa Marekani Patrick Day amefariki baada ya kulazwa siku nne hospitali kwa ajili ya matibabu ya matatizo ya ubongo aliyoyapata katika pambano lake la dhidi ya Charles Conwell jumamosi iliyopita .
Baada ya kuanguka na kupoteza fahamu katika raundi ya kumi, Patrick alikimbizwa hospitali, ambako alifanyiwa upasuaji ambao hata hivyo haukunusuru maisha yake hadi ilipotangazwa jana kuwa amefariki .
Akizungumza kwa masikitiko makubwa kufuatia kifo cha Patrick, Charles Comwell ameungana na wadau wa michezo kote duniani kuomboleza kifo cha bondia huyo mwenye umri wa miaka 27 .
Akijibu salamu za heri kutoka kwa watu mbalimbali duniani kote, Promota Lou Dibella ambaye pia aliwakilisha familia ya Patrick, amewashukuru wadau hao kwa upendo wao tangu Patrick akutwe na matatizo.