Benki ya KCB Tanzania kupitia KCB Biashara Club yapeleka wafanyabiashara 10 kwenda nchini China kwa lengo la kukutana na wazalishaji halisi wa bidhaa mbalimbali ili kujifunza na kutafuta namna bora ya kuweza kuboresha biashara zao.
Wafanyabiashara hao watakaa nchini China kwa siku 10 na kupata fursa ya kutembelea miji miwili mikubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Mahusiano na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye alisema wameanza kuwapeleka China wafanyabiashara hao ambao ni wateja wa benki hiyo ili wakakutane na wazalishaji halisi na siwalanguzi au madalali ambao uwauzia bidhaa kwa bei ya juu.
Amesema kwa muda mrefu wafanyabiashara nchini ambao wanakwenda China wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali ikiwamo za lugha na kuuziwa vitu
bei za juu hivyo kupitia safari hizo wanazoziandaa mambo hayo hayatajitokeza.
“Tatizo kubwa ambalo wafanyabiashara walikuwa wanakutana nalo ni kuuziwa vitu kwa bei ya juu na walanguzi au madalali sasa kupitia safari hii tutawakutanisha na wale wazalishaji halisi ambao wanaviwanda ambapo watapata fursa ya kutembelea viwanda vyao kisha kutoa oda za kutengenezewa bidhaa zao,"
"Lakini pia kuna tatizo la lugha kule, kupitia safari hii tuliyoiratibu sisi KCB Benki tutawapatia wakalimani ambao watatembea nao kila mahali ili kurahisisha mawasiliano yao na wazalishaji hao,” amesema.
Naye Meneja Uhusiano wa Wateja Wadogo na wa Kati wa benki hiyo, Moses Kisaka alisema wanamatumaini kwamba siku hizo 10 wafanyabiashara hao wataweza kuzunguka na kukutana na wazalishaji pamoja na kutumia fursa hizo kufanya manunuzi ya bidhaa zao.
Amesema wafanyabishara hao watakutana na wazalishaji halisi watakaowauzia vitu kwa bei ya chini kuliko ilivyokuwa awali walipokuwa wakienda wenyewe na kukutana na walanguzi waliokuwa wanawauzia vitu kwa bei ya juu.
“Tunafanya hivi kwa lengo la kuwasaidia wapunguze gharama za kupata bidhaa, tunaamini safari hizi zitakuwa ni muendelezo na tunatumaini mwakani kuwapeleka wafanyabiashara wengi zaidi,” amesema Kisaka.
Aidha amesema benki hiyo imeanzisha kitengo cha KCB Biashara Club kwa lengo la kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara mbalimbali na kuzungumza juu ya changamoto na fursa za kibiashara wanazokutana nazo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa wafanyabiashara wanaoenda China, Saada Sipemba amesema safari hiyo itawasaidia kupata fursa ya kuona maonyesho makubwa yanayofanywa na wenye viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo vyombo vya ndani pamoja na mashine.
“Pia itatuwezesha kwenda kujifunza na kukutana na wazalishaji wenyewe bila kupitia kwa madalali wowote hivyo itatusaidia kununua bidhaa kwa bei nafuu na kuja kuziuza nchini kwa bei nafuu pia,” amesema Sipemba
Mkuu wa kitengo wa wateja rejareja Masika Mukule akikabidhi tiketi kwa mmoja wa wafanya biashara wa vipodozi Irene Moshi, wakati wa kuwakabidhi tiketi wateja wa benki hiyo ambao wanakwenda nchi china kukutana na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kuepuka kusumbuliwa na walanguzi wakati wanapokwenda kufanya manunuzi hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya KCB Dar es Salaam. (katikati), Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya KCB, Christine Manyenye .
Mkuu wa kitengo wa wateja rejareja Masika Mukule akikabidhi tiketi kwa mmoja wa wafanya biashara wa Kampuni ya Sadio Tours na Travel Saada Sipemba, wakati wa kuwakabidhi tiketi wateja wa benki hiyo ambao wanakwenda nchi china kukutana na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kuepuka kusumbuliwa nawalanguzi wakati wanapokwenda kufanya manunuzi hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya KCB Dar es Salaam. (katikati), Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya KCB, Christine Manyenye .
Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya KCB, Christine Manyenye (kulia) akizungumza wakati wa kuwakabidhi tiketi wateja wa benki hiyo ambao wanakwenda nchi china kukutana na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kuepuka kusumbuliwa na walanguzi wakati wanapokwenda kufanya manunuzi hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya KCB Dar es Salaam Wengine pichani (watatu kushoto), Mkuu wa Kitengo cha wateja wadago na kati Abdul Juma, Mkuu wa kitengo wa wateja rejareja Masika Mukule pamoja na Mfanya biashara wa Kampuni ya Sadio Tours na Travel Saada Sipemba.
Mkuu wa Kitengo cha wateja wadago na wakati Masika Mukule (watatu kushoto), akizungumza wakati wa kuwakabidhi tiketi wateja wa benki hiyo ambao wanakwenda nchi china kukutana na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kuepuka kusumbuliwa na walanguzi wakati wanapokwenda kufanya manunuzi hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya KCB Dar es Salaam (kulia) Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya KCB, Christine Manyenye, Mkuu wa kitengo wa wateja rejareja Masika Mukule pamoja na Mfanyabiashara wa Kampuni ya Sadio Tours na Travel Saada Sipemba.