Umewahi kujiuliza Diamond Platnumz anavaa madini ya kiasi gani shingoni na mikononi, lakini bila shaka utakuwa unajiuliza kwa nini anaongozana na walinzi wengi.

Babu Tale ambaye ni meneja wa msanii huyo ameeleza ni kwa nini Diamond anaongozana na walinzi wengi.

Ufafanuzi wa Tale umekuja wiki moja baada ya staa huyo kuongozana na walinzi 11 na kuzuia maswali na taharuki kwenye maeneo aliyokuwa akipita ikiwamo kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro Hoteli alipoenda kwa shughuli zake binafsi. “Diamond huwa anavaa vito vyenye thamani ya zaidi ya Sh140 milioni akiwa matembezini, akiwa jukwaani gharama inaongezeka kadri anavyovaa vingi, lakini pia ni mkakati wa kibiashara, yule ni staa na anapaswa anapopita ijulikane anapita nani? Anasema Babu Tale, alipofanya mahojiano na gazeti hili kuhusu suala hilo.

Akitolea mfano Tale anasema cheni ambayo Diamond aliwahi kunyang’anywa akiwa jukwaani mkoani Mtwara, thamani yake ilikuwa Sh40 milioni, unaweza kuona ni hasara kiasi anaweza kupata iwapo hakuna ulinzi wa kutosha.