Baada ya Zari kulalamika Jana October 15, 2019  juu ya taarifa za kupotea kwa vitu vyake vilivyokuwa vikisafirishwa na ndege aina ya Kenya Airways, sasa leo shirika hilo limejibu.

Kwa wale ambao hamjui kilichotokea ni kwamba Zari The Boss Lady alilalamika ameibiwa na shirika hilo vitu vyake vya thamani vikiwemo Perfume alizotumiwa na marafiki zake kutokea Dubai pamoja na nguo.

Sasa Leo October 15, 2019 Shirika hilo limejibu Zari the Boss Lady kupitia mitandao yao na kuyaandika

‘Kwako zari tunatamani kwa wateja wetu wote kuwa na safari nzuri, tumekutafuta ili kuweza kupata maelezo yako ambayo yataweza kutusaidia kuratibu pamoja na uongozi ambavyo vimesafiria katika viwanja vyetu (JHB, JKIA, EBB)  ili kuweza kujua kilichotokea tunasubiria jibu lako’- Kenya Airways


Zari aliwajibu kwa neno ‘Thank you’ kwahiyo inaashiria kuelewana na shirika lakini bado Mashabiki wanaendelea kulitupia lawama kampuni hiyo.