Staa wa muziki wa BongoFleva Ali Kiba, ameiomba Serikali iwatumie vizuri wasanii wake ikiwa kuna jambo muhimu kwa sababu wakifanya hivyo, itakuwa ni rahisi kufikisha ujumbe haraka kwa wananchi wake.


Ali Kiba amezungumza hayo baada ya kufika kisiwani Zanzibar na kuombwa kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana kisiwani humo na Waziri wa Habari Utalii na mambo ya kale ,Thabit Kombo.

"Katika jambo la kitaifa au la umuhimu sana ili kushiriki na wananchi au wanajamii ni lazima serikali iwatumie wasanii kwa sababu ni jambo muhimu, busara na njia mbadala ambayo ni rahisi kwa kuwa sisi tunapendwa na wananchi nina imani hiyo" ameeleza Ali Kiba

"Tumekuwa tukifanya kampeni kwenye nchi tofauti tofauti kwa kutumia wasanii, vita vikitokea wasanii ndiyo wanatuliza, ikitokea majanga au serikali inahitaji msaada fulani kwa wananchi wakitutumia sisi inakuwa wepesi sana kuwatimizia" ameongeza.

Pia amewataka wananchi wote kufanya utalii wa ndani kwa sababu kila mtu ana haki ya kujua kila kitu kinachohusiana na nchi yake.