Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeungana na Serikali kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwenye matayarisho ya kumbukumbu ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo kitaifa mwaka huu itafanyika Lindi katika viwanja vya Mpilipili.

Miamvuli hiyo zaidi ya 1000 iliyotolewa na Airtel itatumiwa na watoto watakaendesha halaiki siku ya kilele cha maadhimisho hayo katika viwanja vya mpilipili Lindi.
 Waziri wa Nnchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (pili kushoto) akipokea miamvuli zaidi ya 1000 kutoka kwa Meneja wa mauzo wa Airtel kanda ya Pwani Zephania Ludigiji kwa ajili ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 20 ya kumbukumbu ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo kitaifa mwaka huu itakuwa Lindi, wakishuhudiwa na Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi (katikati), Naibu Waziri wa kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde na wafanyakazi wengine wa Airtel.
 Waziri wa Nnchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (pili kushoto) akipokea miamvuli Zaidi ya 1000 kutoka kwa Meneja wa mauzo wa Airtel kanda ya Pwani Zephania Ludigiji kwa ajili ya maandalizi ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 20 ya kumbukumbu ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo kitaifa mwaka huu itakuwa Lindi, wakishuhudiwa na Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi (katikati), Menjeja matukio wa Airtel Dangio Kaniki (kushoto).
 Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi (katikati)akitoa neno la shukurani baada ya kukabidhiwa miamvuli Zaidi ya 1000 kwa Waziri wa Nnchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu) Jenista Mhagama na wawakilishi wa Airtel kwa ajili ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 20 ya siku ya kumbukumbu ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo kitaifa mwaka huu itakuwa Lindi, wakishuhudiwa na Naibu Waziri wa kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde (tatu kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Andrew Massawe (wa pili kushoto).
Waziri wa Nnchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (kati) akijaribisha mwamvuli aliokabidhiwa na timu ya Airtel, Maalum kama maandalizi ya maadhimisho ya miaka 20 ya siku ya kumkumbuka ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo mwaka huu kitaifa yatafanyika Lindi, huku wakishuhudiwa na wakishuhudiwa na Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi (pili kulia), Naibu Waziri wa kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde (pili kushoto na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Andrew Massawe (kushoto).