Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya kinyago cha umoja Balozi wa Rwanda hapa Nchini Mhe. Eugene Kayihura ambaye amemaliza muda wake wa Utumishi hapa Nchini. Balozi Kayihura amekuwa Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Rwanda hapa Nchini Mhe. Eugene Kayihura mara baada ya kupata chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa Utumishi hapa Nchini. Balozi Kayihura amekuwa Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akiagana na Balozi wa Rwanda hapa Nchini Mhe. Eugene Kayihura mara baada ya kupata chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa Utumishi hapa Nchini. Balozi Kayihura amekuwa Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amemuaga Balozi wa Jamhuri ya Rwanda nchini Mhe. Eugene Kayihura, ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi.

Akiongea wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana Dar es Salaam Prof. Kabudi alimshukuru Balozi Kayihura kwa kumaliza muda wake wa uwakilishi na kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kudumisha mahusiano kati ya Tanzania na Rwanda katika kipindi chake cha uwakilishi.

Aidha, Mhe. Waziri alielezea kwamba yapo maeneo ambayo nchi hizi mbili zitaendelea kushirikiana kwa ukaribu na maeneo mengine Tanzania itaendelea kubadilishana uzoefu na Rwanda ikiwemo huduma za kusambaza madawa maeneo ya vijijini na TEHAMA.

Kwa upande wake, Mhe. Balozi Kayihura aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kumpa ushirikiano wa kutosha wakati wa kipindi chake cha uwakilishi hapa nchini.

Mhe. Balozi alielezea kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi mbili na alipongeza hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Tanzania imeendelea kuzichukua katika kuimarisha mahusiano hayo. 

Aliongeza kwamba hatua hizo zimefanikisha idadi ya wafanyabiashara wa Rwanda kutumia bandari ya Dar es Salaam kusafirisha mizogo yao kuongezeka hadi kufika asilimia 98.