Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kibakwe alipofanya ziara ya kikazi wilayani Mpwapwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe.
George Simbachawene akifurahia wimbo wa kwaya iliyoandaliwa ktumbuizamkutano wa hadhara aliyofanya akiwa ziarani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. George Simbachawene akihutubia wananchi jimboni Kibwakwe wilayani Mpwapwa.
Wananchi wakimkabidhi zawadi ya mbuzi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu waRais (Muungano na Mazingira), Mhe. George Simbachawene mara baada yakufanya mkutano wa hadhara jimboni Kibakwe wilayani Mpwapwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. George Simbachawene ameagiza wanaoharibu vyanzo vya maji katika maeneoyenye miinuko waondolewe mara moja na kuchukuliwa hatua kali za sheria.

Mhe. Simbachawene ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi wa Vijiji vya Chogola na Makosea wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Mpwapwakatika Jimbo la Kibakwe ambapo alikemea tabia ya baadhi ya watu kukata mitikwenye maeneo yenye miinuko hali inayosababisha uharibu wa vyanzo vya maji.

Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo aliagiza watendaji wa kata navijiji kuweka alama za mipaka kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji yenye umbaliwa urefu wa mita 500 kila upande ili kuhakikisha wananchi hawavivamii.

Tunapokata miti ya asili tunafanya maisha yetu kuwa magumu na vyanzo vya maji vinategemea uhifadhi wa misitu ya asili, inashangaza watu wanafyeka miti hadi kwenye milima kitakachotokea mvua ikinyesha kwa kasi ule udondounaporomoka na kusababisha mmomonyoko wa udongo mtakuta kijiji chotekinasombwa,  alitahadharisha.

Pamoja na hayo Simbachawene alibainisha kuwa changamoto ya mabadiliko yatabianchi imesababisha mabadiliko ya misimu na hivyo kuleta athari kwa wanadamu kushindwa kuendesha shughuli za kilimo.

Aliongeza kuwa hali hii imechangia kubadilisha misimu na ndio maana wananchiwanalalamuka kukosa mvua za kutosha kuweza kufanya shughuli za kilimo. Akiendelea kutoa elimu kwa wananchi Waziri Simbachawene alisema kitendocha kukata miti kinaharibu ikolojia ya wanyama na mimea hali inayosababishakukosekana kwa mvua na hivyo mabadiliko ya tabianchi.

“Tarehe 23 ya mwezi huu (Septemba), Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa marais wote kujadili namna nchi hizi zimezalisha hewa ya ukaa ambayo tunaitakaboni kutokana na shughuli zetu wenyewe.“Hewa ya ukaa imeongezeka na kutengeneza joto gesi ambalo linatoboa anga la dunia ambayo ni (ozoni layer) hali husababisha misimu kubadilika na hivyo ndomaana tunakabiliwa na changamoto ya mabadliko ya tabia nchi”. Alisema waziri huyo.