Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt John Jingu akipokewa na Kamati ya Shule ya Msingi Mnyigumba iliyoko katika Kijiji cha Kitelewasi Kata ya Rungemba nje Kidogo ya Mji wa Mafinga Mkoani Iringa alipowasili Kijijini hapo kwa lengo la kujionea uhamasishaji wa  shughuli za maendeleo zinazotekelezwa kwa pamoja kati ya Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Rungemba na Kijiji hicho.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt John Jingu akiangalia mahindi lishe wakati alipotembelea  Shule ya Msingi Mnyigumba iliyoko katika Kijiji cha Kitelewasi Kata ya Rungemba nje Kidogo ya Mji wa Mafinga Mkoani Iringa alipowasili Kijijini hapo kwa lengo la kujionea uhamasishaji wa  shughuli za maendeleo zinazotekelezwa kwa pamoja kati ya Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Rungemba na Kijiji hicho.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt John Jingu akikagua Mradi wa Kilimo cha parachichi katika Kijiji cha Kitelewasi Kata ya Rungemba nje Kidogo ya Mji wa Mafinga Mkoani Iringa alipowasili Kijijini hapo kwa lengo la kujionea uhamasishaji wa  shughuli za maendeleo zinazotekelezwa kwa pamoja kati ya Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Rungemba na Kijiji hicho.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt John Jingu akizungumza na Wanakijiji cha Kitelewasi Kata ya Rungemba nje Kidogo ya Mji wa Mafinga Mkoani Iringa alipowasili Kijijini hapo kwa lengo la kujionea uhamasishaji wa shughuli za maendeleo zinazotekelezwa kwa pamoja kati ya Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Rungemba na Kijiji hicho.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Na Mwandishi Wetu Mafinga

CHUO cha Maendeleo ya Jamii kilichopo Kata ya Rungemba Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimeleta neema kwa wananchi wanaowazunguka kwa kuhamasisha wananchi wa Vijiji wa Kata hiyo kushiriki katika miradi mbalimbali ya kuwaletea  maendeleo ikiwemo miradi ya lishe bora pamoja na elimu ya kilimo inayowataka kuzingatia kanuni bora za upandaji mazao.


Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Siku moja ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt.John Jingu alipotembelea Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba mkoani Iringa kujionea kasi ya uhamasishaji wananchi kushiriki katika miradi ya kujiletea Maendeleo inayofanywa na Chuo hicho.

Dkt. Jingu amesema kuwa jamii ikishiriki katika miradi ya kiuchumi yenye matokeo chanya maisha ya wananchi yatabadilika kwa haraka sana na kuwezesha wananchi kujikwamua kiuchumi na kuwataka wanachi kutambua kuwa hakuna wakuwaletea maendeleo bali maendeleo yataletwa na wao wenyewe.

Aidha Dkt.Jingu ameridhishwa na kazi ya uhamasishaji wananchi kujiletea Maendeleo kwa wananchi wa vijiji vya Rungemba Itimbo na Kitelewasi ambao tayari wameanza kunufaika kiuchumi badala ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba  kuhamasisha Maendeleo ya kilimo  na lishe bora.

Dkt. Jingu aliongeza kuwa kuwa na elimu ya nadharia bila vitendo haitoshi akaongeza kuwa ni vyema vyuo vingine nchini vikatembelea chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba ili kuiga namna ambavyo Chuo hicho kinatekeleza dhana ya ushirikishaji Jamii katika maendeleo ya Jamii kwa vitendo.

Akizungumzia kuhusu miradi ya uzalishaji Mali katika vijiji vya Kata ya Rungemba Mkulima kutoka Kijiji cha Kitelewasi Bw.Augustino Mbedule amesema kutokana na mafunzo na miradi ya uhamasishaji unaofanywa na Chuo hicho tayari Jamii kijijini hapo imeanza kubadilika kimaisha.

Bw.Mbedule ameitaja miradi ilioanzishwa na Chuo hicho kuwa ni uhamasishaji kilimo cha mahindi lishe, Kilimo cha zao la parachichi, ufugaji nyuki na kampeini ya unyonyeshaji maziwa ya mama ili kupambana na udumavu wa watoto chini ya miaka mitano.


 Mkufunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba Bw. Raphael Mbiiji amesema Chuo hicho kikisaidiana na Chuo Kikuu Cha Sokoine Mjini Morogoro walifanya utafiti katika Vijiji vya Itimbo,Kitelewasi na Rungemba vilivyopo nje kidogo ya mji wa Mafinga Iringa na matokeo ya utafiti huo yalionyesha vijiji hicho kina tatizo kubwa udumavu kwa watoto wachanga.


Bw. Mbiiji aliongeza kuwa na matokeo ya utafiti huo yaliyopelekea Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba pia uhamasisha Jamii za vijiji  kuhusu umuhimu wa kunyonyesha na lishe boraIli kukabiliana na tatizo la udumavu kwa watoto na kwa sasa mwamko wa Jamii katika kilimo cha mahindi lishe na mbogamboga unazidi kuongezeka.


Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu anaendelea na Ziara ya Siku Tano katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kutembelea vyuo vya Maendeleo ya Jamii na pia Makazi ya Wazee yaliyoko katika Mikoa hiyo.