Na Woinde shizza Michuzi Tv, Arusha
WAKAGUZI hapa nchini wameeleza mafanikio ya kupungua kwa ubadhilifu wa Mali za umma kwa kiwango kikubwa katika sekta mbalimbali za serikali na binafsi baada ya serikali kuridhia ukaguzi wa aina moja.

Wameeleza hayo jijini Arusha kwenye mkutano wa sita  wa wakaguzi wakuu wa hesabu za ndani, ulioandaliwa na taaisisi ya ukaguzi wa ndani (IIA)wakidai kuwa mafanikio ni baada ya serikali kupitia bodi ya wahasibu NBAA kuridhia viwango vya kimataif√† vya ukaguzi wa ndani mwaka 2011.

Mkaguzi wa ndani na Mkuu wa serikali msaidizi upande wa ubora wa Ukaguzi wa ndani AIAG(QA),Chotto Sendo amesema kuwa  mafanikio hayo yametokana na maboresho mbalimbali yaliyofanyika ikiwemo wakaguzi wa ndani kutumia ufumo mmoja wa ukaguzi.

Amesema mabadiliko yaliyofanyika yamewezesha wakaguzi wa ndani kuimarika zaidi katika kuibua ubadhilifu unaoendelea na hivyo kupunguza mianya ya hiyo katika taasisi mbalimbali.

"Changamoto kubwa kwa sasa tupo katika hatua ya kuelekea kwenye viwanda lakini tulikuwa hatujajiandaa kulingana na viashiria hatarishi vilivyokuwepo ndio maana tunaendesha haya mafunzo kukabikiana na vihatarishi" Alisema.

Naye Mkurugenzi katika taasisi ya ukaguzi wa ndani,(IIA),Zelia Njeza amesema kuwa wamejikita kutoa elimu kwa wadau na kujielimisha kupitia mafunzo mbalimbali kuhakikisha kwamba wanatoa huduma inayotakiwa kwa maendeleo chanya.

Amesema kuwa kumekuwepo namwamko mkubwa kwa wakaguzi wa ndani katika kusimamia kazi yao na kuongeza usimamizi katika udhibiti wa viashiria hatarishi ,utawala bora na mifumo ya udhibiti.

Kwa upande wake Mkaguzi Mkuu wa ndani wa mamlaka ya viwanja vya ndege Zanzibar, Safia Abdulhamid amesema kuwa changamoto kubwa inayowakabili wakaguzi wa ndani ni kushindwa  kutekelezwa kwa mapendekezo yao baada ya kukamikisha ukaguzi.

Pia amesema wakaguzi wa ndani wamekuwa wakiogopeka na kutazamwa  kama Askari Polisi jambo ambalo linawafanya kupata ugumu katika kutekeleza majukumu yao.