Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya KCB Christina Manyenye, (kulia), akizungumza na wafanyabiashara zaidi 300 wakati wa kongamano la KCB Biashara Club liliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa dhumuni la kutoa mafunzo katika nyanja mbali mbali za kuendesha biashara, fursa ndani ya Biashara Club na utayari wa benki hiyo kuhakikisha kwamba wateja wake wanachukua  fursa hizo.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya KCB, Masika Mukule akijibu swali kutoka kwa mmoja ya wafanyabiashara zaidi 300 wakati wa kongamano la KCB Biashara Club liliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa dhumuni la kutoa mafunzo katika nyanja mbali mbali za kuendesha biashara, fursa ndani ya Biashara Club na utayari wa benki hiyo kuhakikisha kwamba wateja wake wanachukua  fursa hizo.
 Mkuu wa Kitengo Wafanyabishara Wadogo na wa Kati (SME) wa Benki ya KCB, Abdul Juma (kulia), akizungumza na wafanyabiashara zaidi 300 wakati wa kongamano la KCB Biashara Club liliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa dhumuni la kutoa mafunzo katika nyanja mbali mbali za kuendesha biashara, fursa ndani ya Biashara Club na utayari wa benki hiyo kuhakikisha kwamba wateja wake wanachukua  fursa hizo.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Benki ya KCB Tanzania imeendelea kusimama na wafanyabiashara wadogo na wa kati kwa kuandaa kongamano la pili la KCB Biashara Club na kuwaoeta pamoja wafanyabiashara zaidi ya 300.

Programu KCB Biashara Club ilibuniwa na benki hiyo kwa dhumuni la kutoa fursa mbali mbali kwa wafanyabiashara zikiwemo mafunzo ya uendeshaji biashara, kuwapa wafanyabiashara jukwaa la kushirikiana pamoja na kuwakuzia mtandano wa masoko ndani na nje ya Tanzania.

Tangu kuanzishwa kwake, KCB Biashara Club imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kukuza biashara katika seckta ya SME kwa kutoa huduma bora za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wakati yaani (SME) pamoja na kuwaonyesha mbinu za kukuza mitaji ya shughuli zao za kibiashara.

Akizungumzia kongamano hilo, Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Christine Manyenye amesema Benki ya KCB imefanya juhudi za mahususi za kuwaleta wadau kama Injinia Jane Kadoda kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambaye aligusia athari za biashara kwa mazingira pamoja umuhimu wa kutii sheria za kulinda mazingira zilizowekwa na serikali ya Tanzania

Amesema, Mwezi Machi Mwaka 2019, Benki ya KCB iliendesha kongamano kama hili jijini Arusha hususan kwa wafanyabiashara walio katika sekta ya utalii.

Akiongea wakati wa kufungua semina hiyo, Kwa upande wake mdau kutoka European Investment Bank (EIB), Fasili Boniface ameongelea umuhiumu wa kuweka kumbukumbuku za kifedha na jinsi ya kuainisha matumizi ya binafsi na ya kibiashara.

Naye Saada Sipemba ambaye ni mtaalamu wa safari za kibiashara kutoka Sadio Travel and Tourism ameongelea fursa za kibiashara zinazopatikana nchini China na juhudi za benki hiyo kuhakikisha inawatengenezea wateja wake mianya ya kuchukua fursa hizo kwa urahisi.

KCB kupitia Biashara Club imekuwa ikiandalia wadau wake safari za kibiashara kwenda nchi kama China, Malaysia na Afrika Kusini kwa gharama nafuu kwa dhumuni la kuwafungulia masoko mapya na bidhaa nafuu za kuleta kwenye soko la Tanzania.

Mbali na kufaidika na ujuzi wa kupitia semina na safari mbalimbali zinazoandaliwa na KCB Biashara Club, wanachama pia wanafaidika kwa kujenga uhusiano wa kibiashara baina yao unaopelekea kuongeza ujuzi na kupanua wigo wa biashara.

KCB inatambua umuhimu wa wafanya biashara wadogo na wa kati katika kukuza uchumi wa nchi lakini pia inatambua kwamba uchumi hautakuwa kama wafanya biashara hao hawatakuwa na nyenzo sahihi za kibiashara.