Moni Centrozone na mpenzi wake Nai wamepiga stori na EATV & EA Radio Digital na kuelezea mambo makubwa wanayoyafanya kwa sasa pamoja na mipango ya mahusiano yao ikiwemo ya ndoa.


Moni amesema kuwa yeye na mpenzi wake hivi sasa wako 'bize' na mambo makubwa ya kimaendeleo na kwamba hawako kimaigizo kama watu wanavyowafikiria.

“Kwanza mahusiano yetu hayawezi kutajwa kwenye ujinga ndio maana hatuongelewi kwa watu. Tunafanya mambo makubwa yenye maendeleo na kuangalia zaidi mipango yetu, hatutaki maigizo kwa sababu wabongo wanapenda kuongelea mambo mabaya kuliko vitu vya kuleta maendeleo”, amesema Moni.

Aidha Moni ameahidi kufunga ndoa muda si mrefu kutoka sasa, akitoa ahadi kuwa watu wasubiri wakati rasmi ukifika watafanya hivyo,"kuhusu ndoa watu wasubiri muda si mrefu, kwa sababu ndoa sio kitu cha masihara na cha kukurupuka, ni vitu vya kujipanga".