Hisia zimetawala kwa wengi mno katika uwanja wa sanaa ambapo kila mmoja akihusisha vita ya Harmonize na Diamond Platnumz katika kujitoa Wcb. (Hisia)

Ambapo hakuna uhalisia wa kweli katika kujitoa kwa Harmonize chini ya Genge la Wcb, isipokuwa hisia. (Dhanio)

Lakini wengi ni wenye tafakari kuu yakuwa vita hii italeta anguko kwa Ali Kiba. Na katika uhalisia hakuna ukweli katika hilo anguko ambalo wanaliwaza. (Hakika)

Ikumbukwe Ali Kiba si msanii mwenye simamio la Trendi katika kila leo. Bali ukimya wake wenye utofauti hata awali ya ushindani wa kulazimishwa na Diamond. (Muda)

Ila kwa upande wa Wcb na Diamond na Genge  lake ni wenye kupenda trendi zaidi tena za namna yoyote. Na kama ikitokea hakuna trendi basi ni tatizo kwao. (Kabisa)

Ilihali kwa Ali Kiba si msanii wa trendi kabisa, vivyo vita hii kama ni ya kutengeneza au yenye uhalisia ni wazi haiwezi kumtikisa wala kumuangusha Kiba kwa kuwa yukatika njia zake. (Upekee)

Vivyo katika kweli yenye kweli ndani ya uhalisia vita ya Diamond na Harmonize haimuwezi Ali Kiba . (Daima)

Ikumbukwe mikakati ya Ali Kiba si yenye kuhusisha matukio ya kila leo na ambayo ni ya namna yoyote ile. (Uhalisia)

Sasa kama mikakati ya Kiba ni upekee, Je! Vita hii itawezaje kumuangusha Ali Kiba? (Tafakari)

Kiba ataanguka kama ikitokea ni mwenye kubadili mikakati yake na kufanya ya wenzake na kuacha uhalisia wake ambao awali yake ni zoefu la wengi. (Muigo)

Vivyo kama vita itakuwepo eidha ni kweli ama kutengeneza ni wazi haiwezi kumuangusha Ali Kiba. Ila itawaweka wao wenyewe katika yao. (Hakika)

Na ikumbukwe tu yakuwa “Mwenye moja havai mbili” (Daima)