Ni miezi mitatu tu imepita tangu “video vixen” Tunda na msanii wa Bongo Fleva, Whozu waonyeshe mapenzi yao katika mitandao ya kijamii na sasa imeonekana penzi la wawili limeingia dosari baada ya Tunda kuonekana akimuomba msamaha Whozu.


Tunda alipost picha ya keki katika mtandao wa kijamii wa Instagram ambayo iliandikwa “am sorry” kisha kuandikwa ujumbe unaoelezea jinsi anavyojutia kumkosea Whozu.

“Najichukia mimi mwenyewe kwasababu nimemuumiza mtu muaminifu, mzuri, anayenijali ambaye sijawahi kumjua kabla , kama unaweza naomba unisamehe bado nakuhitaji kwenye maisha yangu, nimefanya vitendo  vya kitoto najionea aibu kwa tabia yangu naomba unisamehe, penzi lako ni msukumo wangu usiniache. Kwangu ni fahari kuwa na wewe, nakupenda na unisamehe Whozu”, ameandika Tunda.

Baada ya kuandika hivyo Whozu hakujibu chochote na katika mtandao huo wa Instagram inaonyesha kuwa Tunda hajam-follow mtu yeyote.

Muda mfupi baadaye mashabiki walitoa maoni yao kwa kuandika, “mtu akikiri kosa lake anastahili kusamehewa 'be a gentleman' msamehe mwenzio”, ameandika Miss Everthing94

“Mapenzi ya mastaa bwana yapo kwenye mitandao ya kijamii tu“, Julyne Official

“Unaomba msamaha ushachepuka tayari ama” aliuliza shabiki

EATV & EA Radio Digital tumejaribu kuwatafuta wote wawili ili watolee tamko juu ya kilichotokea kati yao na kinachoendelea kwa sasa lakini hawakuonyesha ushirikiano kwa kutopokea sim