Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania, Shakila Mayumana akizungumza wakati wa kutambulisha mradi huo leo Septemba 28, 2019

TGNP Mtandao imetambulisha rasmi mradi wa Sauti ya Wanamke na Uongozi Tanzania 'Women's Voice and Leadership - Tanzania' utakaotelezwa kwenye mikoa 9 kwa lengo la kujenga uwezo kwa wanawake wa Tanzania, vikundi na Taasisi za kutetea haki za wanawake ili kuwezesha wanawake na wasichana na kuongeza ulinzi wa haki za wanawake na wasichana kufikia usawa wa kijinsia.

Mradi huo utakaodumu kwa kipindi cha miaka mitano 'Aprili 2019 hadi Machi 2023' kwa ufadhili wa Global Affairs Canada (GAC) umetambulishwa rasmi  leo  Jumamosi Septemba 28, 2019 kwa washiriki wa mradi waliohudhuria Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika kikao cha kutathmini Tamasha la Jinsia la 14  kilichofanyika kwenye ukumbi wa TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.


Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Wanawake na Uongozi Tanzania, Shakila Mayumana amesema mradi huo utatekelezwa katika mikoa tisa ambayo ni Dar es salaam, Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Dodoma, Kilimanjaro, Mtwara, Mara na Kigoma.


"Tulichagua mikoa ambako TGNP inafanya kazi zake, lakini pia kwenye maeneo yenye vuguvugu na yale yaliyosahaulika.Na hii inatokana na masuala tunayofanyia kazi ikiwemo sekta ya maji, afya, elimu, kilimo na uziduaji 'mafuta, gesi na madini' na Ukatili wa Kijinsia", alisema Mayumana.


Aliwataja walengwa wakuu katika mradi huo kuwa ni watu binafsi, jamii, taasisi na vikundi vya wanawake na kubainisha kuwa pia makundi ya jamii ya wafugaji, wawindaji na wanaoishi kwa kula matunda, mizizi na asali pia yameongezwa kwenye mradi huo.


Mayumana alitumia fursa hiyo kuitaka jamii kuachana na mila na desturi potofu zinazokandamiza haki za wanawake na kuwahamasisha wanawake kudai haki zao ikiwemo kujitokeza kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi.


Kwa upande wake, Mwanachama wa TGNP Mtandao, Rehema Mwateba alisema mbegu ya mabadiliko inaanzia kwa mtu mmoja mmoja huku akiwasisitiza wanawake kusimamia ukweli katika kudai haki kwani ukweli siku zote unashinda.
Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania,Shakila Mayumana akitambulisha mradi huo kwa  washiriki wa mradi waliohudhuria Tamasha la 14 la Jinsia  2019. Wanaharakati  hao wa haki za wanawake wanatoka mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Shinyanga, Dodoma, Kilimanjaro, Mtwara, Mara na Kigoma.

Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania,Shakila Mayumana akielezea malengo ya mradi huo.Alisema lengo la mradi ni kujenga uwezo kwa wanawake wa Tanzania,vikundi na Taasisi za kutetea haki za wanawake ili kuwezesha wanawake na wasichana na kuongeza ulinzi wa haki za wanawake na wasichana kufikia usawa wa kijisia.
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiandika dondoo muhimu wakati wa kutambulisha mradi wa Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania.
Kulia ni Mwanaharakati wa haki za wanawake na watoto mkoani Mbeya Flora Mlowezi akichangia hoja wakati wa kutambulisha mradi wa wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania. 
Mwanachama wa TGNP Mtandao,Rehema Mwateba akichangia hoja wakati wa kutambulisha mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania. 
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Same mkoani Kilimanjaro,Abdulrahman Mfuru akiwasisitiza wanawake kuomba mikopo inayotolewa kwenye halmashauri ili wainuke kiuchumi.
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa ukumbini wakati wa kutambulisha mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania. 
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa ukumbini wakati wa kutambulisha mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania. 


Wanaharakati wa haki za wanawake wakiandika dondoo muhimu wakati wa kutambulisha mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania.

Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa ukumbini.
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa ukumbini.
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mradi wa wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania kutambulishwa leo Septemba 28,2019 katika ukumbi wa TGNP Mtandao Mabibo jijini Dar es salaam.
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mradi wa wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania kutambulishwa leo Septemba 28,2019 katika ukumbi wa TGNP Mtandao Mabibo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog