TETEMEKO kubwa la ardhi limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 9:30 (usiku wa kuamkia leo) mkoani Katavi na kuyakumba baadhi ya maeneo mkoani humo na mikoa ya jirani.
Kwa mujibu wa mjiolojia kutoka Taasisi ya Jiolojia, Gabriel Mbogoni amesema tetemeko hilo lina ukubwa wa ritcha 5.5 na kilomita 10.
Aidha, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi amesema tetemeko hilo lilidumu kwa dakika tatu huku akieleza kwamba athari zake bado hazijajulikana.