RAPA kutoka pande za Marekani, Tekashi 69, amekiri kutuma kikosi cha wahuni 12 wa kundi lake la zamani la “Nine Trey Gang” na kuwalipa Dola 500 ili kumpora na kumpiga risasi aliyekuwa mlinzi wake  baada ya tukio la yeye kutekwa.

Tekashi alikiri kudanganya kuhusu baadhi ya yaliyotokea kwani alipigwa na kupoteza fahamu kipindi hayo yote yanatokea.

Hata hivyo Tekashi aliieleza mahakama kuwa baada ya kupona alimfuata meneja wake, Mel Murda, nyumbani kwake aliyemwambia mhusika mkuu wa tukio la yeye kutekwa ni Harv.

Tekashi aliongeza kuwa watu hao waliiba vito vyake vya thamani ya  Dola 365 na ujumbe mbalimbali mfupi wa simu zilionyesha wazi kuwa Harv alihitaji kuiba vito hvyo.

Yote hayo yalikuja baada ya ushahidi wa sauti na video zinazothibitisha Tekashi kutuma watu 12 kumdhuru Harv, baada ya Harv kuthibitika kushiriki katika kumpora na kumteka Tekashi.