Vifo vinavyotokea, katika kundi la vijana kati ya miaka 15 hadi 29, kujiua inachukua nafasi ya pili baada ya kwanza ambayo huwa ni ajali.

Dkt.Praxeria Swai, daktari bingwa wa magonjwa ya akili katika hospitali ya taifa nchini Tanzania(Muhimbili) anasema kuwa kuna sababu nyingi ambazo zinapelekea kundi la vijana hawa wanapelekea kutaka kujiua.

Vijana wengi huwa ndio umri wa kubalehe na wanapitia changamoto nyingi, mara nyingi huwa wanajaribu vitu vingi sana katika maisha yao.

Familia na vijana mara nyingi huwa wanakuwa hawaelewi,malumbano mengi, hawana taarifa sahihi na kile kinaweza kutokea na wanataka kujaribu kila kitu kama vilevi.


Lakini pia inawezekana hawana taarifa sahihi ya nini wanapaswa kukifanya wakipitia changamoto ya aina hiyo.

Wengi huwa wana maumivu ya kihisia ndio maana wanapitia katika maamuzi kama hayo.

Vijana wa kiume wanajiua zaidi ya wakike
Wanaume wanaweza kujiua mara tatu zaidi ya wanawake ambao huwa wanaishi na mawazo ya kutaka kujiua mara tatu zaidi ya wanaume.

Wanaume wachache sana wanajaribu kujiua na kupona, wengi huwa hawaponi.

Katika kituo cha Muhimbili , Dkt. Swai anasema kuwa kuna kiwango kikubwa sana cha vijana wanaokuja na tatizo la sonona na afya ya akili.

Kila baada ya sekunde 40 mtu mmoja mahali fulani, wanajikatiza uhai duniani.

Watu takribani 800,000 hufa kwa kujikatiza uhai wao kila mwaka kwa mujibu wa Shirika la afya duniani (WHO) na ni sababu ya pili ya vifo miongoni mwa watu wenye umri kati ya miaka 15 na 29, nyuma ya vifo vitokanavyo na ajali za barabarani.

WHO inasema kuwa tatizo hili halijazungumzwa vya kutosha miongoni mwa jamii za watu.

Vitendo hivi huathiri watoto, wazazi, wenza na marafiki.