Shilole awafungia kazi Roma na Stamina kisa wimbo wao ‘Kijiwe Nongwa’ kumkosea heshima mume wake Uchebe.

Shilole amedai kuwa amesikitishwa kutajwa Kwenye wimbo huo Kama Mdangaji Wakati yeye ajawahi kudanga na kusema kuwa aijamuuma sana yeye kuibwa ila imemuuma Sana mumewe kusemwa vibaya katika wimbo huo.

 “Wamenisema mm mdangaji mimi niliwahi kudanga jamani wamenivunjia heshima sana ila nawaambia Romalishaaa na Staamina wakibishana na mimi wanakuwa wanaume kama mabinti”