WAKATI watu wakikwepa majukumu kutokana na ugumu wa maisha, mwanamitindo Jane Rimoy ‘Sanchi’ yeye anasaka watoto mapacha kwa gharama yoyote. Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Sanchi alisema anatamani mno kupata watoto mapacha hivyo ana mpango wa kupandikiza watoto hao, baada ya hapo atulie kwa ajili ya kuwalea vizuri.

“Nime-shafanya michakato ya kujua hospitali gani ninaweza kufanya zoezi la kupandikiza watoto mapacha hivyo kila kitu kinaenda sawa, kwa kweli furaha yangu itakamilika nikishawapata tena nipate wa kike na kiume, nitakuwa na amani zaidi,” alisema Sanchi.