Rubani mwanafunzi amefanikiwa kutua salama na ndege baada ya mwalimu wake kuzirai akiwa mitamboni nchini Australia.

Max Sylvester, aliwasiliana kwa dharura na waelekezi wa ndege saa moja baada ya mwalimu wake kuzirai wakiwa angani siku ya Jumamosi.

Alipoulizwa kama anajua jinsi ya kupaisha ndege aina ya Cessna, alijibu: "Hili ni somo langu la kwanza".Wahudumu hao walimsaidia kutua ndege salama katika uwanja wa ndege wa Perth.