Baada ya Rais wa Tanzania, John Magufuli kumwagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhakikisha miradi ya ujenzi wa Coco Beach na machinjio ya Vingunguti yenye thamani ya  Sh26.

Hatimae Makonda ameunda kamati maalumu  kusimamia utekelezaji wa miradi ya kimkakati katika mkoa huo ambayo itahusisha wataalamu mbalimbali wakiwemo maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Makonda ametoa kauli hiyo leo katika hafla ya utoaji udhamini kwa wanafunzi wa kike 100 wanaosoma masomo ya Sayansi lakini wazazi wao hawana uwezo wa kuwasomesha.

Amesema kamati hiyo itaongozwa na katibu tawala wa Mkoa na itahusisha wataalamu wa sekta mbalimbali za ujenzi, ununuzi, uhasibu na maofisa wa Takukuru,   kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi inayoanzishwa kwenye halmashauri za Dar es Salaam.

"Watendaji wa halmashauri watatakiwa kutoa ripoti kwenye kamati hiyo kila baada ya wiki mbili, mara mbili kwa mwezi. Hatuwezi kuwa tunacheleweshwa na wanasiasa kwenye halmashauri zetu," amesema Makonda.