Rais Donald Trump wa Marekani amesema amefuta mkutano wa faragha na mwenzake wa Afghanistan Bw. Ashraf Ghani na mwakilishi wa Kundi la Taliban uliopangwa kufanyika leo huko Camp David, nchini Marekani baada ya shambulizi dhidi ya askari wa Marekani kutokea nchini Afghanistan.

Kwa mujibu wa rais Trump, rais Ghani na viongozi wa Kundi la Taliban walipanga kuwasili Marekani tarehe 7 usiku.

Lakini alifuta mkutano huo pamoja na mazungumzo ya amani baada ya kundi la Taliban kukiri kuwajibika na shambulizi lililotokea tarehe 5 mjini Kabul, ambalo lilisababisha kifo cha askari mmoja wa Marekani na wengine 11 kujeruhiwa.