Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping kwa kuuendeleza ushirikiano na uhusiano mzuri wa Tanzania na China ikiwemo misaada na uwekezaji ambao China inaufanya hapa nchini.

Rais Magufuli ametoa shukrani hizo leo katika hafla ya makabidhiano ya magari 40 kutoka Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) kwenda Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyofanyika katika Makao Makuu ya JWTZ Upanga Jijini Dar