Mhispania Rafa Nadal ameshinda ubingwa wa US Open 2019 baada ya kumfunga Mrusi Daniil Medvedev kwa seti 7–5, 6–3, 5–7, 4–6, 6–4 katika mchezo wa fainali.

Nadal,33, sasa ameshinda ubingwa wa US Open kwa mara ya nne na hii ni Grand Slam yake ya 19 kuchukua, moja nyuma ya Roger Federer mwenye 20.