Mkongwe wa rap nchini Marekani, Dana Elaine Owens maarufu kama Queen Latifah ameibuka na kuwataka mashabiki wamuache Nicki Minaj apumzike kwa furaha na amani kwani amefanya mengi katika tasnia ya muziki kabla ya kutangaza kustaafu.

Kwa mujibu wa mtandao wa TM, mkali huyo amesema kuwa anaamini siku moja Nick atarudi kwenye muziki japo amekuwa kwenye tasnia hiyo kwa muda mrefu, “bado muda anao wakufanya mengi zaidi kwenye tasnia hii na kurudisha kwa jamii” alisema mkali huyo

Wiki iliyopita rapa Nicki Minaj aliandika ujumbe katika ukurasa wake wa twetter na kusema kuwa ameamua kuacha muziki na kuanzisha familia, “naamini mashabiki zangu mtakuwa na furaha muendelee kuniunga mkono mpaka kifo changu” aliandika rapa huyo.

Kupitia ukurasa wake wa tweeter Minaj aliomba radhi kwa mashabiki wake na kusema kuwa ujumbe huo ulikuwa ni wa  ghafla na usiojali hisia za watu wake na kuahidi kutatolea ufafanuzi kauli hiyo kupitia kipindi chake cha Queens Radio